Thursday, March 22, 2018

Updates: Mbowe, Mwalimu Wameachiwa Kwa Dhamana......, Heche na Mnyika washikiliwa, Mdee na Matiko wanasakwa..


Viongozi watatu  wa Chadema walioripoti Kituo Kikuu cha Polisi wakiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji wameachiwa kwa dhamana huku wawili wakitakiwa kubaki.

Viongozi walioachiwa ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu na Dk Mashinji.

Mwalimu amesema Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Serengeti, John Heche wamebaki polisi kwa maelezo kuwa wamekuwa wakikwepa taratibu za dhamana.

Heche na Mnyika hawakuripoti polisi Machi 16, 2018 huku chama hicho kikieleza kuwa moja ya sababu ya wabunge hao kutoripoti ni kutokana na kuhudhuria vikao vya kamati za Bunge mjini Dodoma.

Dk Mashinji ameeleza kuwa viongozi wengine wa chama hicho waliotakiwa kuripoti polisi leo akiwemo mbunge wa Kawe, Halima Mdee wamepata dharura.

Hata hivyo,  Jeshi la Polisi limetoa amri kuwa Wabunge hao, Halima Mdee na Ester Matiko wakamatwe popote walipo na kufikishwa Polisi kwa mahojiano.

No comments:

Post a Comment