Na Paschal Dotto-MAELEZO
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Rais Mstaafu (Awamu ya Tatu), Mhe.
Benjamin William Mkapa ametangaza uteuzi wa Profesa Egid Beatus Mubofu
kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, nafasi iliyokuwa inashikiliwa na
Profesa Idris Suleiman Kikula.
Uteuzi
huo umetangazwa rasmi tarehe 5, Machi 2018 kupitia taarifa iliyotolewa
kwa vyombo vya habari na ofisi ya Mkuu wa UDOM, Mhe. Benjamin Mkapa.
Kabla
ya uteuzi huo Profesa Mubofu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Viwango Tanzania (TBS), na kabla ya hapo alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi wa Profesa Mubofu unaanza rasmi tarehe 17 Machi, 2018.
Profesa
Idris Kikula ni miongoni mwa wanazuoni waandamizi wanaoheshimika ndani
na nje ya nchi kitaaluma kwa kushiriki katika tafiti mbalimbali za
kisayansi na kijamii
Ameshiriki
katika tafiti hizo kwa kushirikiana na taasisi nguli za kitafiti hapa
nchini kama REPOA, pamoja na taasisi ya UONGOZI.
UDOM
ndio chuo kikuu pekee chenye uwezo mkubwa wa kuchukua wanafunzi wengi
hapa nchini na Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara na inakadiriwa kina
uwezo wa kuchukua wanafunzi takriban 40,000, pia kina eneo la ukubwa wa
hekari zaidi ya 6000.
No comments:
Post a Comment