Waziri
Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo amemwakilisha Rais John Magufuli
katika sherehe za kusaini mkataba wa kulifanya Bara la Afrika kuwa eneo
huru la biashara jijini Kigali, Rwanda.
Tanzania
ni miongoni mwa nchi zaidi ya 50 ziilizosaini mkataba huo, ambao
umeelezwa utaongeza chachu kwa Afrika kuimarika kiuchumi.
Mkataba
huo umesainiwa baada ya kukamilika kwa kamati za wataalamu
zilizoshirikisha pia mawaziri wa biashara na mambo ya nje wa nchi
washirika.
Mbali
na mkataba huo, marais hao pamoja na wawakilishi wa nchi washirika
wamesaini Itifaki ya utekelezaji wa makubaliano hayo ambayo yanatoa
uhuru wa makazi, kutembea, haki ya kuishi na kufanyakazi popote Afika
bila vikwazo wala vizuizi sambamba na Tamko la Kigali.
Sherehe
hizo pia zimehudhuriwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald
Mengi na Mwenyekiti wa CEO Round Table, Ally Mufuruki ambaye jana
alikuwa miongoni mwa wazungumzaji katika mjadala wa uchumi na biashara.
No comments:
Post a Comment