Mwanariadha nchini
Afrika Kusini nusura akatwe miguu kabisa aliposhambuliwa na kundi la
wanaume alipokuwa anafanya mazoezi Jumanne alfajiri.
Polisi
wanasema mwanaraidha huyo hakuwafahamu wanaume waliomshambulia lakini
inavyoonekana ni kwamba shambulio hilo sio la wizi wa kawaida, na kwa
hivyo maafisa wanachunguza uwezekano wa njama nyingine.
Mwanariadha
Mhlengi Gwala mwenye umri wa miaka 26 anapokea matibabu katika
hospitali moja huko KwaZulu-Natal baada ya kushambuliwa na wanaume
watatu katika mji wa pwani Durban.
Haijulikani dhamira ya
shambulio hilo lakini polisi wanasema mwanariadha Gwala aliwapa
washambuliaji simu na pesa alizokuwa nazo, ambao badala yake walimsukuma
chini na kumburura katika kichaka kilichokuwa karibu na kujaribu
kumkata miguu yake kwa kutumia msumeno usiokuwa na makali.
Msemaji wa polisi Nqobile Gwala ameiambia BBC kwamba uchunguzi umeanzishwa wa jaribio la mauaji.
Amekitaja kisa hicho kama cha "kushutusha na chenye kuvunja moyo".
Mkasa huo umewatia wasiwasi raia wengi nchini Afrika kusini - hata iwapo ni nchi inayoshuhudia visa vingi vya uhalifu.
Marafiki zake Gwala , wanaowasiliana na madakatari wanaomtibu, wanasema atapona kikamilifu lakini taratibu.
Hata hivyo atahitaji kufanyiwa upasuaji.
Wengi wanatumia mitandao ya kijamii kushinikiza kukamtwa kwa wahalifu hao na wapewe hukumu nzito gerezani.
No comments:
Post a Comment