Jeshi
la polisi mkoa wa Dodoma limewakamata na kuwashikilia watu wawili kwa
tuhuma za kuhamasisha maandamano kwenye mitandao ya kijamii
yanayotarajiwa kufanyika April 26 mwaka huu.
Kamanda
wa polisi wa mkoa Dodoma Gilles Muroto amesema watu hao wamekua
wakisambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu
kuandamana huku wakijua ni kosa kisheria.
Aidha
Kamanda Mruto ametoa wito kwa watu kutofuata mkumbo kuhamasisha watu
kufanya maandamano kwani ni kosa kisheria na kuwa yeyote ambaye
atakamatwa atashughulikiwa kisheria.
"Watu
hawa wamekuwa wakihamasisha wananchi kufanya maandamano, tulishasema
Serikali haijalibiwi leo tunaanza kutoa mifano kwao. Wale wote
wanaoijaribu Serikali tutahakikisha tunawachukulia hatua za hali ya juu
sana”
Mbali
na hilo Kamanda Mruto amesema kuwa upelelezi ukikamilika watu hao
watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao kuhusu kuhamasisha watu
kufanya maandamano kupitia mitandao ya kijamii ambayo yamepangwa
kufanyika April 26, 2018 nchi nzima na yakiratibiwa na mwanadada Mange
Kimambi kupitia mitandao ya kijamii.
No comments:
Post a Comment