Huu
ni mkanda wa video wa kwanza kutolewa na Shekau baada ya kimya cha miezi kadhaa
iliyopita, naye ni mongoni mwa viongozi wanaosakwa kwa hamu na ghamu na kupewa
sifa ya kuwa miongoni mwa magaidi wanaosakwa na Marekani pamoja na mamlaka ya
Nigeria.
Abubakar
Shekau anaonekana kwenye mkanda huo wa video akiwa ameketi peke yake akiwa
amevalia kanzu,kofia yenye rangi inayofanana na bunduki aina ya AK-47 ambayo
anaonekana kuwa na mahaba nayo.Lakini anaonekana
kushindwa kuzungumza kwa sauti yenye mamlaka ikilinganishwa na matamko yake ya awali .
kushindwa kuzungumza kwa sauti yenye mamlaka ikilinganishwa na matamko yake ya awali .
Akisoma
kutoka katika karatasi kwa lugha ya kiarabu na ki Hausa, Shekau, anakiri kundi
lake kuhusika katika matukio ya hivi karibuni nchini Nigeria katika maeneo ya
kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo ikiwemo lile lililotukia siku ya siku kuu ya
Christimas katika kijiji cha Molai nje ya jiji la Maiduguri, mji mkuu wa Jimbo
la Borno.
Shekau
alijinasibu kwa kusema kuwa askari wa kundi la wanamgambo la Boko Haram wana
afya maridhawa na kwamba vikosi vya ulinzi nchini Nigeria haviwezi kufanya
lolote dhidi ya wanamgambo wake.
Sehemu
ya dakika thelathini na moja ya mkanda huo zimeoneshwa mbwembwe za wapiganaji
wa kundi hilo ikiwemo magari ya silaha, malori na pikipiki huku wakinapiga
risasi hewani kwa kile kinachoonekana kizuizi cha njiani katika kambi ya
kijeshi iliyotelekezwa .
Wakati
huo huo Shekau alionekana akitoa tamko juu ya kukerwa kwake dhahiri juu ya
kutambuliwa hivi karibuni mji wa Yerusalemu kama mji mkuu wa Israeli tamko
lililotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump, Abubakar Shekau, ameijosoa nchi
ya Saudi Arabia kwa kushirikiana na wale aliowaita makafiri na kuwalaumu
Wapalestini kwa uharibifu wao.
Mpaka
sasa serikali ya Nigeria haijatoa tamko lolote juu ya mkanda huo wa video na
ujumbe uliomo ndani yake. Hata hivyo jeshi la Nigeria linakiri kuwafukuza waasi
kutoka katika ngome zao kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo, hata hivyo
wanamgambo wa kikundi cha wapinaji cha Boko Haram bado wanaendeleza
mashambulizi ya kujitoa muhanga , mashambulizi ya risasi za moto zaidi wakilenga
vifaa vya kijeshi na vijiji.
No comments:
Post a Comment