Mtu
mmoja nchini Kenya mwenye umri wa miaka 35 amefikishwa mahakamani
akituhumiwa kubaka mbuzi wawili wa jirani yake, na kisha kuwaua.
Tukio
hilo limetokea Januari 13 mwaka huu, baada ya watu kumuona akiwaburuza
mbuzi hao kutoka porini ambako anahisiwa kufanya tukio hilo, katika eneo
la Kangundo
Waendesha
mashtaka wametaka mbuzi hao wapelekwe kufanyiwa vipimo ili kubaini kama
kweli wamefanyiwa kitendo hicho, na kutaka mshtakiwa kupatiwa matibabu
baada ya kulalamika alipigwa vibaya na polisi walipoenda kumkamata.
Kesi hiyo imehairishwa mpaka Januari 29, na mshtakiwa kupewa dhamana ya shilingi 100,000 za Kenya.
Sheria za Kenya zinamtaka mtu atakayekutwa na hatia ya kufanya ukatili kama huo kwa wanyama kwenda jela kwa miaka 14.
No comments:
Post a Comment