Mjumbe
wa Kamati Kuu Chadema, Edward Lowassa ametoa ufafanuzi kuhusu
mazungumzo yake na Rais John Magufuli yaliyofanyika Ikulu Dar es Salaam
siku sita zilizopita.
Kupitia
taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo Januari 15, 2015,
Lowassa amesema alimueleza masuala mbalimbali yanayowakumba wananchi na
wanasiasa tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani.
“Nilijadiliana
naye kuhusu masuala mbalimbali ya msingi kuhusu nchi yetu ikiwemo
kutoheshimiwa kwa Katiba na sheria, uminywaji wa demokrasia, ukiukwaji
mkubwa wa haki za binadamu,” amesema na kuongeza,
“Unaohusisha
kupotea kwa watu, kuvamiwa, kutishwa na kushambuliwa kwa viongozi wa
kisiasa wa upinzani na hali ngumu ya uchumi kwa wananchi wetu. Ni imani
yangu kwamba Rais atayazingatia na kufanyia kazi masuala haya kwa
masilahi yetu.”
Kupitia barua hiyo, Lowassa amesema yupo madhubuti kuliko wakati mwingine wowote ule.
No comments:
Post a Comment