Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, ametangaza kiama
kwa wamiliki ardhi ambao hawajalipa kodi ya pango la ardhi na kutoa
muda hadi April 30 mwaka huu kuhakikisha wanalipa kodi hiyo.
Waziri
Lukuvi ameyasema hayo kwenye ziara mkoani Mwanza alipotembelea
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Halmashauri ya jiji la Mwanza na
kuziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zoezi hilo la ukusanyaji
wa kodi ya pango la ardhi linakamilika kwa wakati.
Amewataka
wakuu wa idara za ardhi nchini kusajili hati za viwanja kwa wanaohitaji
ardhi kwa kutumia majina yanayotambulika kwenye vitambulisho vya taifa
NIDA ili kuepuka udanganyifu ambapo kodi hiyo ipo kisheria.
Waziri
Lukuvi pia amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanapima
maeneo yote yakiwemo mamlaka za viwanja vya ndege, hifadhi za wanyama na
misitu taasisi zinazomiliki ardhi na wizara zote kupimwa.
No comments:
Post a Comment