Friday, January 5, 2018

NABII MKUU MH DK. GEORDAVIE AKABIDHI MSAADA WA CHAKULA KATIKA VITUO VITATU VYA WATOTO YATIMA.

Nabii mkuu Mh Dk GeorDavie amekabidhi msaada wa chakula katika vituo vitatu vya watoto yatima vya christiani women Orpanage care, Themi Youth Orphanage pamoja na Jane Levolosi Orphans Centre wenye thamani ya Tsh. Million 3 na laki sita
Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya  nabii mkuu , Balozi wa nabii mkuu Mtume Sekela Ntondolo amesema kuwa vitu walivyokabidhi katika vituo hivyo ni
pamoja na  Mchele, sukari na  mafuta ya kupikia vilivyotolewa na watu mbalimbali katika sikukuuu ya kukusanya.
Ameongeza kuwa tunapotoa na kuwasapoti watoto yatima na mungu anafungua milango ya Baraka katika mwaka mzima kwa kutopungukiwa  na fedha pamoja na chakula.
Kwa upade wa viongozi wa vituo hivyo wameshukuru kwa msaada huo huku wakiongeza kwa kusema kuwa  Huduma ya ngurumo ya upako imekuwa msaada mkubwa katika vituo vya watoto yatima.
Aidha Balozi Wa Nabii Mkuu Mtume Sekela Ntondolo amesema kuwa sikukuu ya kukusanya bado inaendelea na itafikia tamati tar 31 mwezi huu wa kwanza huku akiwataka watu wengine ambao bado hawajaleta sadaka ya sikukuu ya kukusanya kuleta sadaka zao.


No comments:

Post a Comment