Monday, January 15, 2018

Zaidi ya 1500 wahamishwa baada volkano kulipuka Papua New Guinea

The remote island volcano of Kadovar spews ash into the sky in Papua New Guinea, January 6, 2018

Karibu watu 1,500 wamehamishwa kutoka visiwa vya Papua New Guinea, ambapo mlima ambao umekuwa umetulia kwa muda mrefu ulianza kulipuka, kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu.

Volkano katika kisiwa cha Kodovar ilianza kutoa moshi na majivu wiki iliyopita, na kusababisha kuhamishwa kwa zaidi ya watu 500 kwenda kisiwa kilicho karibu cha Blup Blup.
Baada ya mlipuko kuzidi sasa wale waliokimbilia kisiwa cha Kodovar sasa watahamishiwa kwingine.
Papua New Guinea ni nyumbani kwa milima kadhaa ya volkano.

No comments:

Post a Comment