Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Comoros, Azali Assoumani,
kwenye ndege ya shirika la Ethiopian Airline, wakiwa safarini kueleke
Ethiopia, katika Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika
AU, Waziri Mkuu, anamwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano
huo. Januari 28, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga, wakati
alipo wasili kwenye uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Addis Ababa,
kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu
wa Nchi za Umoja wa Afrika AU Nchini Ethiopia. Januari 28, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini, Jacob
Zuma, kwenye hafla ya miaka 100 ya kumkumbuka Rais wa kwanza wa Afrika
Kusini, Nelson Mandela, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Sheraton, Mjini
Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia kumwakilisha Rais John
Pombe Magufuli kwenye Mkutano huo. Januari 28, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisainiwa kitabu cha kumbukumbu, cha Rais wa
kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela na Rais wa Afrika Kusini, Jacob
Zuma, kwenye hafla ya miaka 100 ya kumkumbuka Kiongozi huyo,
iliyofanyika kwenye Hoteli ya Sheraton, Mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu
yupo Nchini Ethiopia kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye
Mkutano huo. Januari 28, 2018.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
No comments:
Post a Comment