Jeshi
la Polisi nchini limetiliana saini mkataba wa makubaliano na Jeshi la
Polisi la Msumbiji kushirikiana kupambana na uhalifu katika nchi hizo
mbili, hasa maeneo ya mpakani.
Mkataba
huo utahusisha kubadilishana taarifa, mbinu na uzoefu katika kupambana
na ugaidi na dawa za kulevya ambazo zinaathiri nguvu kazi kwenye mataifa
yao.
Akizungumza
na vyombo vya habari leo Januari 15, 2015 kabla ya kusaini makubaliano
hayo, Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Simon Sirro amesema wahalifu
waliodhibitiwa katika maeneo ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji sasa
wamekimbilia Msumbiji.
Hata
hivyo, amewaonya wahalifu hao kwamba hata huko hawatakuwa salama kwa
sababu Jeshi la Polisi Tanzania linashirikiana na Msumbuji katika
kupambana na uhalifu kwa kubadilishana taarifa.
"Wale
wahalifu waliokimbilia Msumbiji au Congo hawako salama. Majeshi yetu ya
polisi yanashirikiana, ndiyo maana leo tunatiliana saini makubaliano ya
ushirikiano," ameaema Sirro.
Amewataka
wahalifu hao waliokimbilia Msumbiji kuachana na uhalifu kwa sababu
wakiendelea watakamatwa kwa ushirikiano wa majeshi hayo.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi la Msumbiji, Bernardino Rafael
amesema nchi yake inakabiliwa na wahalifu kutoka nchi nyingine, hivyo
makubaliano hayo yatasaidia kupunguza uhalifu.
Amesema wanataka kudhibiti mipaka yao dhidi ya wahalifu hao ambao wanahatarisha amani katika nchi hiyo pamoja na nchi za jirani.
"Watu
wenye ualbino wanauawa kwa imani za kishirikina na taarifa zinaonyesha
wahalifu hao wanatoka mataifa mbalimbali. Tutashirikiana na Polisi
Tanzania katika kubadilishana taarifa ili kukomesha mauaji hayo,"
amesema Rafael.
No comments:
Post a Comment