Papa Farancis ameanza ziara yake
nchini Chile huku kukiwa na wasiwasi wa kutokea shambulizi,kufuatia
tishio lililotolewa kupitia vipeperushi vilivyo tolewa katika shambulio
la
awali kabla ya kuanza kwa ziara hiyo.
Kiongozi huyo wa Kanisa
Katoliki Dunian alipokelewa kwa shangwe na zaidi katika uwanja wa
Santiago mji mkuu wa nchi hiyo,ambapo waumini wa kanisa
Katoliki,viongozi mbali mbali wakiongozwa na rais wa Chile Michelle
Bachelet walikuwepo pia.
Taifa la Chile lina zaidi ya asilimia 60
ya raia wake ni wakristo kati yao asilimia 45 ni wakatoliki,huku taifa
hilo likiwa la pili katika bara la Amerika ya kusini kwa kuwa na idadi
ya watu wasio na dini.
Hata hivyo ziara hii ya Papa nchini Chile
imetanguliwa na matukio ya kushambuliwa kwa mabomu makanisa matatu mji
mkuu wa taifa hilo Santiago huku washambuliaji wakiacha vipeperushi
kwamba shambulio linalofuata ni dhidi ya Papa,kutokana na matukio hayo
rais Bachelet amesema hayo ni matukio ya kushtusha.
Hii ni ziara
yake ya kwanza nchini Chile tangu kuchaguliwa kwake,ziara hiyo
ikikumbana na upinzani mkubwa kufuatia kashfa udhalilishaji wa kingono
dhidi ya watoto unaodaiwa kufanywa na baadhi ya makaaisisi wa kanisa
hilo nchini Chile.
Papa Francis leo anatarajiwa kukutana na
waathirika wa ukatili wa kijeshi uliofanywa na dikteta Augusto
Pinochet,ambapo pia zaidi ya nusu milion wanatarajiwa kuwa katika
mkuasanyiko katika maeneo ambayo Papa atayatembelea katika ziara
yake.Papa Francis amewasili nchini Chile ikiwa ni mwanzo wa ziara yake
ya wiki moja nchini humo pamoja nan chi ya Peru.Sherehe za kumkaribisha
Papa zimefanyika uwanja wa ndege wa Santiago.
No comments:
Post a Comment