Mwanamume anayeshukiwa kutoroka
kutoka eneo la tukio la ajali ya gari ya kutisha iliyowauwa vijana
watatu wa kiume anasakwa na polisi.
Wahanga hao watatu wa
ajali waliokufa baada ya gari la Audi kupandaukingo wa barabara mjini
London, wametambuliwa kama Harry Louis Rice, George Wilkinson na
Josh Kennedy.
Bibi yake George alizulu eneo la ajali katika mji wa Hayes, magharibi mwa London, akasema kuwa familia "imeumia".
Mwanamume
huyo mwenye umri wa miaka , 28, ambaye alikuwa ndani ya gari lilipopata
ajali , ameshikiliwa kwa tuhuma za kusababisha vifo na uendeshaji gari
hatari .
Polisi imesema kuwa inaaamini walau mwanamume mmoja alikimbia baada
ya ajali hiyo kutokea katika bara bara ya Shepiston Lane, ijumaa.
Kijana mwenye umri wa miaka 28 alikamatwa na umma kabla kuwasili kwa polisi, kwa mujibu wa walioshuhudia kisa hicho.
Wachunguzi hata hivyo hawajabaini iwapo kuna uwezekano wa kuwemo kwa
wasafiri zaidi katika gari hilo jeusi aina ya Audi ,ambalo linaaminiwa
kuwa lilikuwa likisafiri kwa kasi kubwa kabla ya kugonga ukingo wa bara
bara kutoka kwenye kituo cha mafuta ya petroli cha Esso..
Waliokufa wawili walikuwa na miaka 16 na mmoja miaka 17, na
walikuwa njiani kusherehekea siku ya kuzaliwa kwenye uwanja uliopo
karibu wa soka.
Babu yake George Wilkinson , Nigel Goodhand, alikwenda kwenye eneo la tukio Jumamosi .
"Nimevunjika moyo sana. Inaumiza.
"lengo langu halikuwa kukomea hapa, lakini nimelazimika hatimae", alisema.
"Nimekasirika, lakini nimeridhika nimekuona. Tutamkosa sana ."
Taarifa
ya polisi mjini London imesema kuwa: "Uchunguzi unaendelea kubaini
kikamilifu mazingira ya ajali na idadi ya watu wahusika''
No comments:
Post a Comment