Mkurugenzi
Mkuu wa CZ Information & Media Consultant LTD, Cyprian Majura
Nyamagambile leo January 15, 2018 amezungumza na waandishi wa habari na
kueleza kuwa yeye na baadhi ya Wanasheria nchini katika siku mbili
zijazo watamfungulia mashtaka Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.
Ameeleza
kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na maneno aliyoyatoa Lissu kabla ya
kwenda nchini Ubelgiji kwaajili ya matibabu, kwa kutoa kauli nzito kuwa
Tanzania kwasasa sio mahali salama pa kuishi na eneo hatarishi kwa
maisha ya binadamu.
Musiba
ameeleza kuwa kauli hizo zililenga kuidhalilisha nchi, kuwapa hofu
wageni wanaokuja nchini kwa ajili ya kutalii lakini pia kuwaogopesha
wananchi washindwe kufanya kazi zao kwa amani na hivyo wanahitaji
aisaidie nchi kutoa uthibitisho wa kauli zake hizo katika vyombo vya
sheria.
“Tunampa
siku mbili atoe uthibitisho wa kauli zake vinginevyo tutampeleka
mahakamani, na japokuwa tutampeleka katika mahakama za ndani, nakala
yake itapelekwa The Hague Uholanzi kwenye Mahakama ya Kimataifa.”
Amesema Cyprian Musiba
No comments:
Post a Comment