Wednesday, January 17, 2018

Afrika Kusini yamwita balozi wa Marekani Kufuatia Matamshi ya Kuudhii ya Rais Donald Trump

Wizara  ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa nchini Afrika Kusini imemwita Naibu Balozi wa Marekani, jijini Pretoria kufuatia matamshi ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo kuhusu nchi za Afrika.


Rais Trump anaripotiwa kuyataja mataifa ya Afrika kuwa machafu wakati wa mahojiano yake kuhusu sera za uhamiaji.

Amewaambia waandishi wa habari kuwa yeye sio mbaguzi.

Taarifa kutoka ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini inasema kuwa inaunga mkono taarifa iliyotolewa na Muungano wa Afrika.

Au ilielezea mshangao wake kutokana na matamshi hayo na kumtaka Trump kuomba msamaha.

Afrika Kusini inasema kuwa uhusiano wake na Marekani unastahili kuwa katika misingi ya heshima.

Namibia, Botswana na Ghana ni baadhi ya nchi ambazo zimetoa taarifa za kumshutumu vikali Rais Trump. 

Credi: BBC

No comments:

Post a Comment