WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma nchini wasijihusishe
na vitendo vya wizi, ufisadi kwani Serikali haitosubiri kuwaundia tume
za kuwachunguza bali itawashughulikia hapo hapo.
Amesema
Serikali haikotayari kuwavumilia watumishi wanaojihusisha na wizi,
ubadhilifu, rushwa na uzembe, hivyo ni vema viongozi waliopewa dhamana
wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa uadilifu.
Waziri
Mkuu alitoa kauli hiyo jana jioni (Jumatatu, Januari 15, 2018) wakati
akizungumza na watumishi wa wilaya ya Musoma mkoani Mara akiwa katika
siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku sita mkoani hapa.
“Fedha
zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali
ya maendeleo zinalenga kutatua kero za wananchi na si kuwanufaisha
wachache wenye tamaa. Kama ni za ujenzi wa zahanati ijengwe na
atakayezitafuna Serikali haitosita kumchukulia hatua.”
Waziri
Mkuu asiwasisitiza watumishi wa umma kufanya kazi kwa mujibu wa sharia
kwa sababu vitendo vya wizi, uzembe vinachangia kupunguza kasi ya
kuwaletea maendelea maendeleo Watanzania.
Alisema
lengo ni kuhakikisha azma ya Serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi
hususan ni wale wa hali ya chini inatimia, hivyo aliwaagiza viongozi wa
halmashauri wakiwemo Madiwani kusimamia vizuri miradi ya maendeleo.
Pia
Waziri Mkuu aliwataka wakuu wa idara na watendaji wengine wa
halmashauri kuacha tabia ya kukaa ofisini na dabala yake waende vijijini
kwa ajili ya kuwafuata wananchi na kushirikiana nao katika kutatua kero
mbalimbali zinazowakabili.
Waziri
Mkuu alisema watendaji hao wanatakiwa waachane na tabia ya kuwasubiri
wananchi wawapelekee malalamiko yao kwa sababu baadhi yao hawana uwezo
wa kufika katika ofisi zao.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
No comments:
Post a Comment