Rais wa Marekani Donald Trump amekiri kuwa mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati ulikuwa katika hali ngumu jana, na kutishia kukata msaada wa Marekani kwa Wapalestina, wa zaidi ya dola milioni 300 kwa mwaka.
Trump aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa iwapo Wapalestina
hawapo tayari kuendelea na mazungumzo ya amani na Israel, hakuna haja ya kuendelea kutoa malipo hayo makubwa kwao.
Trump aliingia madarakani akijisifu kwamba atafanikisha makubaliano ya mwisho katika kanda ya Mashariki ya Kati, jambo ambalo limewashinda marais wote wa Marekani tangu mwishoni mwa miaka ya 1960.
Amekuwa akiwashinikiza Wapalestina kufikia makubaliano, kwa kutishia kufunga ubalozi wao mjini Washington, kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, na kuachana na sera ya miongo kadhaa ya Marekani.
Kwa sehemu kubwa ya nusu karne iliyopita, Marekani imekuwa ikionekana kama mpatanishi asiepingika wa mchakato wa amani ya Mashiriki ya Kati. Lakini vitendo vya Trump vinazidi kuitia mashakani hadhi hiyo.
No comments:
Post a Comment