Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amemsaidia mama mjane Benadetha
Rwendela aliedhulumiwa nyumba yake Plot No. 239 Block B Kunduchi Beach
kwa kupigwa mnada na madalali kutoka kampuni ya Nkanya Ltd kinyume na
taratibu kisha kuamrishwa kuondoka ndani ya siku 30.
Baada
ya RC Makonda kuona taarifa hizo kwenye baadhi ya vyombo vya vabari na
mitandao alimuita mjane huyo ofisini kwake kisha kumkutanisha na
wanasheria wa mkoa na kubaini utapeli mkubwa uliotumika kuuza nyumba
hiyo kutokana na watu kufoji nyaraka ikiwemo sahihi ya mwenyekiti wa
mtaa huku nyumba hiyo ikiwa na zuio la Mahakama.
Aidha
imebainika kuwa hati za nyumba hiyo zilifojiwa kisha kutumika kuchukuwa
mkopo wa shilingi bilioni moja pasipo mmiliki wa nyumba kujua
kinachoendelea.
Kutokana
na hilo RC Makonda ameagiza Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam Lazaro Mambosasa kuwakamata matapeli waliohusika pamoja na
kuagiza kusimamishwa mnada huo kwakuwa ni batili huku akimsihi mama
mjane kuishi kwa amani kwenye nyumba yake.
Aidha
RC Makonda amesema Jumatatu ya wiki ijayo atakutana na Bank ya KCB kwa
ajili ya mazungumzo huku akiwaagiza madalali wote wanaotaka kufanya
minada kwenye mkoa huu kuhakikisha wanapata ruhusa kutoka kwa wakuu wa
wilaya.
Kwa
upande wake mjane huyo Benadetha Rwendela ameishukuru Serikali ya awamu
ya tano kwa kuwajali wananchi wake na kuwasaidia pale wanapopata
matatizo huku akimpongeza Rais Magufuli kwa kumteua RC Makonda.
No comments:
Post a Comment