Sunday, January 28, 2018

London: Mshukiwa aliyewagonga vijana 3 atorotoka eneo la ajali'

Kuanzia kushoto : George Wilkinson, Harry Louis Rice a na Josh Kennedy

Mwanamume anayeshukiwa kutoroka kutoka eneo la tukio la ajali ya gari ya kutisha iliyowauwa vijana watatu wa kiume anasakwa na polisi.
Wahanga hao watatu wa ajali waliokufa baada ya gari la Audi kupandaukingo wa barabara mjini London, wametambuliwa kama Harry Louis Rice, George Wilkinson na Josh Kennedy.

Waziri Mkuu Majaliwa Awasili Nchini Ethiopia,kumwakilisha Rais Magufuli Katika Kongamano La Viongozi Wakuu Wa Umoja Wa Nchi Za Afrika

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Comoros, Azali Assoumani, kwenye ndege ya shirika la Ethiopian Airline, wakiwa safarini kueleke Ethiopia, katika Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU, Waziri Mkuu, anamwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano huo. Januari 28, 2018.

Waziri Lukuvi Atangaza Kiama

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, ametangaza kiama kwa wamiliki ardhi ambao hawajalipa kodi ya pango la ardhi na kutoa muda hadi April 30 mwaka huu kuhakikisha wanalipa kodi hiyo.

BREAKING NEWS:MKUU WA MKOA WA ARUSHA MH MRISHO GAMBO AKUTANA NA NABII MKUU TANZANIA MH DK GEORDAVIE LEO JUMAPILI.

 


"Jioni Hii ya Leo tarehe 28/01/2018 Mkuu Wa Mkoa Wa Arusha Mh Mrisho Gambo ,Amekutana Na Nabii Mkuu Mh Dk Geordavie Katika Hoteli Ya The Arusha By Sheraton Ili Kusalimiana Na Kupokea Baraka Za Kinabii".

Wednesday, January 17, 2018

Japan yaonya kuhusu urafiki ambao umeonekana kutoka Korea Kaskazini

Kim Jong-un


Japan imeuambia mkutano wa kimataifa kuhusu Korea Kaskazini kuwa dunia isifumbwe macho na urafiki amabo umeanza kuonekana kutoka kwa Korea Kaskazini.

Afrika Kusini yamwita balozi wa Marekani Kufuatia Matamshi ya Kuudhii ya Rais Donald Trump

Wizara  ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa nchini Afrika Kusini imemwita Naibu Balozi wa Marekani, jijini Pretoria kufuatia matamshi ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo kuhusu nchi za Afrika.

Rais Magufuli Akutana na Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo Na Kupiga Marufuku Michango Yote Shuleni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Januari 17, 2018 amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za Serikali za msingi na Sekondari na kuwaagiza Mawaziri Jafo na Ndalichako kusimamia hilo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya January 17

SIJARIDHISHWA NA UJENZI WA KITUO CHA SIRARI-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hajaridhishwa na ubora wa ujenzi wa kituo cha forodha cha Sirari kilichopo kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya.

Papa Francis aanza ziara nchini Chile huku kukiwa na hali ya wasi wasi

Papa Francis akiwa ziarani nchini Chile,Amerika ya kusini.


Papa Farancis ameanza ziara yake nchini Chile huku kukiwa na wasiwasi wa kutokea shambulizi,kufuatia tishio lililotolewa kupitia vipeperushi vilivyo tolewa katika shambulio la

Watoto waliofungwa minyororo wapatikana kwenye nyumba California

David Allen Turpin (left) and Louise Anna Turpin
Wazazi wawili wamekamatwa huko California baada ya polisi kupata watu 13 waliokuwa wameshikiliwa m

Watu 20 wameuawa katika mapigano Libya

Mashambulizi yanayofanywa Libya


Watu 20 wameuawa kufuatia mapigano yaliyotokea kati ya makundi ya wanamgambo hasimu katika mji mkuu wa Libya, Tripoli

Hofu baada ya samaki mwenye sumu kali kuuzwa Japan

Fugu fish


Mji mmoja nchini Japan umetangaza onyo la dharura kuzuia watu kula samaki anayejulikana kama Fugu baada ya samaki huyo mwenye sumu kali kuuzwa kimakosa.

Atiwa Mbaroni Kwa Kubaka Mbuzi Wawili wa Jirani Yake

Mtu mmoja nchini Kenya mwenye umri wa miaka 35 amefikishwa mahakamani akituhumiwa kubaka mbuzi wawili wa jirani yake, na kisha kuwaua.

RC Makonda amfuta machozi mjane ambaye nyumba yake iliuzwa na matapeli

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amemsaidia mama mjane Benadetha Rwendela aliedhulumiwa nyumba yake Plot No. 239 Block B Kunduchi Beach kwa kupigwa mnada na madalali kutoka kampuni ya Nkanya Ltd kinyume na taratibu kisha kuamrishwa kuondoka ndani ya siku 30.

Waziri Mkuu Asema Serikali Haitasubiri Kuwaundia Tume Wezi na Mafisadi......Asisitiza kwamba atakayebainika atashughulikiwa hapo hapo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma nchini wasijihusishe na vitendo vya wizi, ufisadi kwani Serikali haitosubiri kuwaundia tume za kuwachunguza bali itawashughulikia hapo hapo.

Monday, January 15, 2018

SEKTA YA MADINI LAZIMA IWE NA MCHANGO MKUBWA KWENYE PATO LA TAIFA: MHE DOTTO BITEKO

Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akizungumza na wakuu wa idara na vitengo pamoja na wafanyakazi wote wa wizara ya madini mara baada ya kuwasili ofisini Mjini Dodoma, Leo Januari 15, 2018. Picha Zote Na Mathias Canal.

Zaidi ya 1500 wahamishwa baada volkano kulipuka Papua New Guinea

The remote island volcano of Kadovar spews ash into the sky in Papua New Guinea, January 6, 2018

Karibu watu 1,500 wamehamishwa kutoka visiwa vya Papua New Guinea, ambapo mlima ambao umekuwa umetulia kwa muda mrefu ulianza kulipuka, kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu.

Dari la jengo la soko la hisa laanguka Jakarta

An ambulance arrives at the Indonesian Stock Exchange building following reports of a collapsed structure inside the building in Jakarta


Dari la jengo la jengo liliko soko la hisa mjini Jakarta limeanguka na

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya January 15 kwa hiyo kama hukupata nafasi ya kununua gazeti soma hapa kwa kina

Serikali yatoa ufafanuzi Kuzuia matumizi fedha za kigeni

Serikali imesema haijazuia matumizi ya fedha za kigeni nchini bali imechukua hatua ya kudhibiti matumizi ya fedha hizo kulinda thamani ya shilingi ya Tanzania.

Rais Magufuli aomboleza vifo vya watu 11 Kagera

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kufuatia watu 11 kupoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Nyangozi, Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera.

Afrika Kusini yamuita balozi wa Marekani kufuatia matamshi ya Trump kuhusu Afrika

AU ilieezea mshangao wake kutokana na matamsh hayo na kumtaka Trump kuomba msamaha.


Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Afrika Kusini imemuita naibu balozi wa Marekani mjini Pretoria kufuatia matamshi ya Trump kuhusu nchi za Afrika.
Bwana Trump anaripitiwa kuyataja mataifa ya Afrika kuwa machafu wakati wa mahojiano kuhusu sera za uhamiaji.

Kiongozi wa UKIP amtema mpenzi aliyesema watu weusi wana sura mbaya

Henry Bolton and Jo Marney



Kiongozi wa chama cha UKIP nchini Uingereza Henry Bolton anasema kuwa amesitisha uhusiano na mpenzi wake baada ya yeye kuripotiwa kutoa maoni ya ubaguzi wa rangi kumhusu Meghan Markle.

Jeshi la Polisi Tanzania na Msumbiji watiliana saini ya makubaliano Kuzuia Uharibifu

Jeshi la Polisi nchini limetiliana saini mkataba wa makubaliano na Jeshi la Polisi la Msumbiji kushirikiana kupambana na uhalifu katika nchi hizo mbili, hasa maeneo ya mpakani.

BREAKING: Lowassa afunguka kilichompeleka Ikulu

Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, Edward Lowassa ametoa ufafanuzi kuhusu mazungumzo yake na Rais John Magufuli yaliyofanyika Ikulu Dar es Salaam siku sita zilizopita. 

Cyprian Musiba atangaza kumshitaki Tundu Lissu

Mkurugenzi Mkuu wa CZ Information & Media Consultant LTD, Cyprian Majura Nyamagambile leo January 15, 2018 amezungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa yeye na baadhi ya Wanasheria nchini katika siku mbili zijazo watamfungulia mashtaka Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

Thursday, January 11, 2018

SERIKALI YAKIRI KUINGIZWA MKENGE UBINAFSISHAJI TTCL.....DR MPANGO AKABIDHI RIPOTI YA UCHUNGUZI KWA RAIS MAGUFULI

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango jana tarehe 11 Januari, 2018 amewasilisha taarifa ya kamati aliyoiunda kuchunguza umiliki wa kampuni ya simu Airtel kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyeagiza kufanyika kwa uchunguzi huo tarehe 20 Desemba, 2017.

Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo, Dkt. Mpango amesema Serikali imejiridhisha

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO IJUMAA, JAN12,2018


Sunday, January 7, 2018

WAZIRI MPINA AKAMATA KILO 65,600 ZA SAMAKI ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI MIA TATU

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina amekamata kilo 65600 za samaki wachanga aina ya Sangara waliokaushwa kwa chumvi wenye thamani ya shilingi milioni mia tatu katika Kisiwa cha Lubili wilayani Muleba kwenye Mkoa wa Kagera baada ya wamiliki wa samaki hao kukimbia.
Akizungumza leo na Waandishi wa Habari katika Ofisi ya Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera, Mpina amesema tukio la kukamatwa kwa samaki hao lilifanikiwa baada kupata taarifa kutoka kwa raia

SAA ZAHESABIKA MSAKO WA MTUHUMIWA KIFO CHA MKE.

Jeshi la Polisi limesema msako dhidi ya Mhasibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Ami Lukule, ambaye anatuhumiwa kwa mauaji ya mkewe, kichanga chake na shemejiye wa kike, unaendelea vizuri na wanaamini kuwa watamtia mbaroni wakati wowote.

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMATATU, JAN 08,2018


Friday, January 5, 2018

NABII MKUU MH DK. GEORDAVIE AKABIDHI MSAADA WA CHAKULA KATIKA VITUO VITATU VYA WATOTO YATIMA.

Nabii mkuu Mh Dk GeorDavie amekabidhi msaada wa chakula katika vituo vitatu vya watoto yatima vya christiani women Orpanage care, Themi Youth Orphanage pamoja na Jane Levolosi Orphans Centre wenye thamani ya Tsh. Million 3 na laki sita
Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya  nabii mkuu , Balozi wa nabii mkuu Mtume Sekela Ntondolo amesema kuwa vitu walivyokabidhi katika vituo hivyo ni

Thursday, January 4, 2018

MBARONI KWA KUTAPELI FEDHA ZA RAIS

Kijana mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Mohamedy Msangi (28) mkazi wa Kilakala Manispaa ya Morogoro anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kughushi nyaraka na kujipatia mkopo wa milioni 15 katika taasisi ya mfuko wa Rais Kanda ya Morogoro.


HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JAN 05,2018


Tuesday, January 2, 2018

UBOVU MAGARI MAPYA YA POLISI WAISHITUA WIZARA MAMBO YA NDANI.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imebaini madudu katika utekelezaji wa mkataba wa uagizaji wa magari 777 kwa ajili ya Jeshi la Polisi yaliyoagizwa kwa gharama za dola za Marekani milioni 29.77 (Sh. bilioni 66.288).

Kutokana na hali hiyo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad

TRUMP ATISHIA KUWAKATIA MSAADA WAPALESTINA.

Rais wa Marekani Donald Trump amekiri kuwa mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati ulikuwa katika hali ngumu jana, na kutishia kukata msaada wa Marekani kwa Wapalestina, wa zaidi ya dola milioni 300 kwa mwaka. 
Trump aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa iwapo Wapalestina

NABII MKUU TANZANIA MH DK. GEORDAVIE ATEMBELEA MADUKA YA AIM MALL ILI KUTIMIZA NENO LA KINABII LA MWAKA 2018.

Nabii mkuu Mh Dk. GeorDavie  amefanya ziara ya kutembelea maduka ya AIM MALL jijini Arusha kama ishara ya kutimia kwa neno la kinabii la mwaka 2018 lisemalo ni mwaka wa kuvuka mipaka ya malengo yako.
Image may contain: 5 people, people standing

HATUA ILIYOFIKIWA NA SERIKALI KATIKA UNUNUZI WA TRENI MPYA ZA KISASA.

Serikali kupitia Kampuni Hodhi ya Reli (RAHCO) imetangaza mchakato wa awali wa zabuni ya ununuzi wa vichwa na mabehewa kwa ajili ya treni ya umeme itakayotumika katika reli ya kisasa (Standard Gauge) ambayo ujenzi wake unaendelea.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO, Masanja Kadogosa ameithibitishia Idara ya Habari (MAELEZO) kuanza kwa mchakato huo ambao unafuata taratibu za kimataifa za ununuzi kwa njia ya ushindani.

Kwa mujibu wa tangazo la zabuni, jumla ya vichwa 14 vya treni ya umeme kwa

ABUBAKAR SHEKAU AIBUKA TENA NA UJUMBE.

Kiongozi wa kikundi cha wapiganaji wa Boko Haram Abubakar Shekau, ameonekana kwenye video mpya karibu saa ishirini na nne baada ya Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kwa mara ingine kutamka hadharani kuwa kikundi hicho kimesambaratishwa.
Huu ni mkanda wa video wa kwanza kutolewa na Shekau baada ya kimya cha miezi kadhaa iliyopita, naye ni mongoni mwa viongozi wanaosakwa kwa hamu na ghamu na kupewa sifa ya kuwa miongoni mwa magaidi wanaosakwa na Marekani pamoja na mamlaka ya Nigeria.
Abubakar Shekau anaonekana kwenye mkanda huo wa video akiwa ameketi peke yake akiwa amevalia kanzu,kofia yenye rangi inayofanana na bunduki aina ya AK-47 ambayo anaonekana kuwa na mahaba nayo.Lakini anaonekana

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JAN03,2018.