Monday, February 12, 2018

ANTONIO CONTE AKUNWA NA MASHABIKI CHELSEA IKISHINDA

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte, amewapongeza mashabiki wa timu hiyo kwa kumuunga mkono, baada ya jana kupata ushindi mzuri wa magoli 3-0 dhidi ya West Bromwich katika dimba la Stamford Bridge.

Mustakabali wa kocha Conte katika Chelsea umekuwa ukikabiliwa na misukosuko baada ya kupoteza michezo kwa kipigo kizito kutoka kwa Bournemouth na Watford, ila kwa ushindi wa jana imerejea katika nafasi ya nne.

Matokeo hayo mazuri kwa Chelsea na kwa kocha Conte katika kutetea kibarua chake, yametokana na magoli yaliyofungwa jana na Eden Hazrad aliyefunga magoli mawili na Victor Moses akafunga goli moja.
          Eden Hazard akiachia shuti na kufunga goli kati ya magoli yake mawili aliyofunga jana
Victor Moses akishangilia kuwa kuruka sarakasi baada ya kufunga goli huku kipa wa West Bromwich akiwa amekaa chini asiamini

No comments:

Post a Comment