Waziri
wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amelitaka jeshi la polisi kufanya
kazi kwa uadilifu mkubwa na kwamba taasisi hiyo ndiyo inayoshughulika
na haki za watu na wasipofanya kwa uadilifu yapo madhara makubwa kwa
jamii na kutoka kwa wahalifu.
Akizungumza
katika uzinduzi wa ujenzi wa Kituo cha polisi Wilaya ya Pangani jana,
Dk Mwigulu alisema kuwa wilaya ya Pangani ni lango ambalo wahalifu hasa
wahamiaji haramu hupitia kwenda kusini mwa Tanzania.
‘’Kamateni
wahalifu wote wanaoingia kimagendo au wanaoingiza mizigo kimagendo
hakuna mjadala kamateni na wafikisheni katika vyombo vya sheria
,’’alisema Dk Mwigulu.
Kwa
mujibu wa Dk Mwigulu, Mikoa ya kaskazini mwa Tanzania inaongoza kwa
kuingiza wahamiaji haramu na bidhaa kwa magendo kwasababu ipo mipakani
hivyo kuamua kuchangia vifaa vya ujenzi ili kuunga mkono juhudi hizo.
‘’Ujenzi
huu wa kituo cha polisi utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama zaidi
hivyo mimi nitachangia nondo 150 baada ya mifuko 450 ya cement
kupatikana basi ujenzi uanze haraka iwezekanavyo na kituo kiwe cha hali
ya juu kikubwa.’’ alisisitiza
Kwa
upande wake, Mkuu wa Polisi wilaya hiyo, Mrakibu Mwandamizi wa polisi
Christina Musyani amesema kuwa wilaya hiyo ina vituo vitatu pekee vya
polisi ambavyo havitoshi na mazingira yake hayaridhishi.
Alisema
wameamua kuanza ujenzi wa kituo hicho ili kurahisisha utoaji wa huduma
kwa wakazi wa eneo hilo ambao kwa sasa hulazimika kusafiri umbali mrefu
kutafuta vituo vya polisi.
"Kwa kushirikiana na wananchi, Mbunge na halmashauri tumeamua kuanza ujenzi wa kituo cha kisasa ,’’ alisema Christina.
No comments:
Post a Comment