Mwanasiasa
wa muungano wa upinzani nchin Kenya Nasa, Miguna Miguna amefurushwa na
kupelekwa nchini Canada kupitia ndege ya KLM , kulingana na wakili wake Nelson
Havi na Cliff Ombeta.
Bwana
Ombeta amesema kuwa aliarifiwa kwamba bwana Miguna aliingizwa katika ndege
iliokuwa ikielekea Amsterdam na baadaye kuelekea Canada.
"Ni
kweli .Alilazimishwa kuingia katika ndege ya KLM dakika chache tu kabla ya saa
nne usiku na tumebaini kwamba anaelekea Canada. Ni ukiukaji mkubwa wa haki'',
alisema Dkt Khaminwa kwa simu.
Haijulikani
ni sheria gani iliotumiwa na serikali kumuondoa nchini Kenya kwa kuwa katiba
inampatia haki kama raia wa Kenya kwa kuwa ni mzaliwa wa taifa hilo.
Anasema
kwamba wakati Miguna alipokamatwa , serikali ya Canada ilikuwa imeiandikia
Kenya kionyesha wasiwasi kwamba raia wake alikuwa ananyanyaswa na walitaka
arudishwe nchini humo.
Bwana
Miguna siku ya Jumanne alielezea vile alivyokamatwa bila mawasiliano na familia
yake ama wakili wake kwa siku tano.
Alisema
kuwa maafisa wa polisi walimnyanyasa kwa kumfungia katika maeneo ambayo hayafai
kwa binaadamu.
Ripoti
za kufurushwa nchini Kenya zilijiri saa chache baada ya jaji wa mahakama kuu
Luka Kimaru kumzuia mkurugenzi wa Ujasusi na inspekta jenerali wa polisi dhidi
ya kumwekea mashtaka yoyote.
Image caption Kiongozi
wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga akila kiapo cha kuwa rais wa wananchi
Jaji
huyo awali alikuwa ameamuru kwamba inspekta jenerali wa polisi na mkurugenzi wa
shirika la ujasusi walikuwa wamekiuka agizo la mahakama lililowataka
kumwachilia kiongozi huyo.
Huku
Jaji huyo wa Kajiado akiagiza awasilishwe mbele ya jaji Kimaru katika mahakama
ya Milimani, bwana Miguna hakuwasilishwa katika mahakama hiyo huku mawakili
wake wakilazimika kusubiri hadi usiku wakisubiri kuachiliwa kwake.
Miguna
alikamatwa Ijumaa iliopita huku jaji wa mahakama kuu James Wakiaga akimwachilia
kwa dhamana ya ksh. 50,000 lakini hakuachiliwa.
Mkurugenzi
wa shirika la ujasusi baadaye alisema kuwa bwana Miguna alikamatwa baada ya
kukiri kumpatia kiapo kiongozi wa Nasa Raila Odinga mbali na kuwa mwanachama wa
kundi lililopigwa marufuku la NRM.
No comments:
Post a Comment