NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mtwara
WAANDISHI wa Habari za uchumi na Fedha, wameaswa kutumia kalamu zao vema ili kuongeza tija katika jitihada za serikali za kujenga uchumi wa viwanda nchini ifikapo mwaka 2025, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt.Julian Raphael Banzi amesema leo Februari 5, 2018 wakati akifungua semina ya waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha kwenye ukumbi wa BoT , mkoani Mtwara.
“Waandishi mnao wajibu wa kuamsha ari ya uelewa kwa wananchi kuwaelimisha nini serikali inafanya kwa ajili ya nini na kwa utaratibu upi.”
Alisema
Dkt. Banzi na kuwaasa badala ya waandishi kutumia muda mwingi kuandika
maswala ambayo hayasaidii sana katika kusaidia ujenzi wa uchumi, ni vema
sasa wakaangazia katika kuelimisha umma juu ya jitihada za serikali
wakati huu ambapo kuna utekelezaji wa miradi mbali mbali ya kiuchumi
kama vile jenzi wa reli ya kisasa, (SGR).
Naibu
Gavana pia amewataka waandisjhi wa habari kuwafichua wale wanaokatisha
tama au kukwamisha uwekezaji nchini kwani kwa kutofanya hivyo waandishi
wa habari watakuwa hawawatendei haki wananchi na umma kwa ujumla.
Alisema
kuwa BoT inaposema pato la taifa limeongezeka, haimaanishi kwamba
wananchi wanajazwa pesa mfukoni lakini pia mwananchi inabidi ajiulize
yeye mwenyewe anashiriki vipi katika ujenzi wa uchumi ili kuweza
kufaidika na pato lenyewe.
“Kwa
msingi huo elimu mtakayopata hapa katika kipindi cha siku tano,
itawaongezea uwezo wa kufanya uchambuzi wa kina mnapoandika makala ze
uchumi, biashara na fedha ili ziweze kuufikia umma kwa usahihi na
kuepuka upotoshaji.” Alisema Dkt. Banzi.
Kwa
upande wake, Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Itifaki cha BoT, Bi. Zalia
Mbeo, alisema semina hii ni ya tano ambazo BoT imekuwa ikifanya kila
mwaka, ili kujenga uelewa kwa waandishi kuweza kuandika kwa usahihi
shughuli za BoT.
“Tumezidi
kuona mafanikio makubwa tangu tuanze kutoa semina kwa waandishi wa
habari kwa waandishi wamekuwa wakijitahidi kuandika kwa usahihi taarifa
za BoT.” Alisema.
Bi Mbeo
pia alisema katika semina ya mwaka huu, waandishi watapata fursa ya
kuelimishwa mambo mbalimbali kutoka Kurugenzi ya sera na tafiti za
uchumi, kurugenzi ya masoko ya fedha, kurugenzi ya usimamizi wa
,mabenki, kurugenzi ya huduma za kibenki na kurugenzi ya mifumo ya
malipo, na pia kuna ushiriki kutoka kurugenzi ya bima ya amana.
“Mwaka
huu tuna kurugenzi ya Katibu wa Boadi ambayo itaelezea dawati ambalo
linashughulikia matatizo ya watu wanayoyapata katika huduma mbalimbali
za kibenki, na kwa kupitia waandishi wa habari, tunategemea wataelimisha
umma kuhusu dawati hili.” Alisema Bi. Mbeo.
Naibu
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Julian Raphael Banzi, akitoa
hotuba ya ufunguzi wa warsha kwa waandishi wa habafri za Uchumi,
Biashara na Fedha, mkoani Mtwara leo Februari 5, 2018. Wengine pichani
kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Itifaki, Benki Kuu ya
Tanzania, Bi. Zalia Mbeo na Mwenyekiti w aSemina, Bw. Ezekiel Kamwaga,
Baadhi ya waandishi wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi.
No comments:
Post a Comment