Rais
wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Jacob Zuma ametangaza kujiuzulu nafasi
yake, baada ya kushinikizwa na chama chake cha African National Congress
(ANC).
Kamati
Kuu ya ANC ilikutana Jumanne na kumtaka Rais Zuma ajiuzulu kabla ya
kuisha kwa siku ya Jumatano, kutokana na tuhuma mbalimbali za rushwa
zilizokuwa zikimkabili.
Mapema
jana mchana Rais Zuma alifanya mahojiano na kituo cha runinga cha
Afrika Kusini na kusema kwamba hawezi kujiuzulu kwa sababu wale wote
wanaomtaka ajiuzulu hawajaweza kumwambia ni kosa gani amefanya.
Kama
Rais Zuma asingejiuzulu, Bunge la nchi hiyo leo Alhamisi lingepiga kura
ya kutokuwa na imani na Rais, ambapo kama matakwa ya sheria yangetimia,
basi Rais Zuma angeng’olewa madarakani.
Akilihutubia
taifa, Rais Zuma amesema kwamba hataki kuona chama tawala, ANC
kinagawanyika ikiwa chanzo ni yeye, hivyo ameamua kujiuzulu nafasi hiyo
aliyoitumikia tangu mwaka 2009.
Rais Zuma aliingia madarakani baada ya mtangulizi wake Thabo Mbeki kujiuzulu kufuatia kushinikizwa na chama chake.
Kufuatia kujiuzulu kwa Zuma, kiongozi wa ANC, Cyril Ramaphosa anatarajiwa kuapishwa kuchukua nafasi ya kuliongoza taifa hilo.
Licha
ya kuchukua uamuzi wa kujiuzulu, Rais Zuma amesema kwamba hakubaliani
na namna ANC walivyoshubghulikia suala lake, kwani kwa miaka yote
aliyokuwa madarakani amewatumikia raia wa Afrika Kusini kwa uwezo wake
wote.
No comments:
Post a Comment