Kamanda
wa Polisi Kinondoni, Murilo Jumanne Murilo amefunguka na kusema kuwa
jeshi hilo sasa linachunguza kauli alizotoa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa
kuhusu kifo cha Kiongozi wa CHADEMA kata ya Hananasif, ambaye mwili wake
uliokotwa ukiwa na majeraha.
Kamanda
Murilo amesema haya jana Februari 14, 2018 wakati akiongea na
waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali ikiwepo suala la uchaguzi na
kusema kuwa wao kama jeshi la polisi wanachunguza taarifa alizotoa
Mbowe kuhusu sakata la kifo cha kiongozi huyo wa CHADEMA.
"Moja
ya kazi kubwa ya jeshi la polisi ni kuchunguza jambo hiyo ni kauli yeye
ametoa na kauli yake tunaichunguza pia anasema hivyo kwa kuzingatia
misingi ipi ambayo inamsukuma yeye kusema hayo anayoyasema...
"Hatuwezi
kuacha mtu akajisemea vitu kwa kusukumwa na hisia zake ndiyo maana sisi
jambo linapotokea jambo la kwanza kabisa kufanya ni kuchunguza....
hatusukumwi na hisia za mtu kwa sababu tunajua yeye hajasomea kazi ya
polisi na hayo anayotamka tunayachukua kama taarifa zingine za kawaida
ambazo mwananchi yoyote anaweza kutupa" alisema Murilo
Aidha Murilo aendelea kudai kuwa wamekuwa wakimsikia sana Mbowe akitoa kauli mbalimbali
"Mhe.
Mbowe tunamfahamu sana amekuwa akitoa matamko mengi mbalimbali hivyo
jukumu letu ni kuchunguza itakavyo lazimika sisi tutamuomba atueleze
anamaanisha nini kutamka hivyo itakavyolazimika lakini hatuwezi
kusukumwa na kauli yake, tukatoka kwenye msingi wa upelelezi na
kuburuzwa na hisia zake halafu baadaye tukosee ili haki isitendeke.
Nachoweza kusema wahalifu wote tukichunguza na kuthibitisha huwa
wanakamatwa"
No comments:
Post a Comment