Taifa la Korea Kaskazini
linatarajiwa kuandaa maadhimisho ya 70 ya gwaride la jeshi lake kabla ya
kufanyika kwa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi nchini Korea
Kusini.
Gwaride la kila mwaka la Pyongyang linaloadhimisha
kuanzishwa kwa jeshi la Korea Kaskazini limekuwa likifanywa kila mwezi
Aprili kwa kipindi cha miaka 40.
Hatahivyo vyombo vya habari
nchini humo vilitangaza mapema mwaka huu kwamba tarehe ya kufanyika kwa
gwaride hilo la kijeshi imebadilishwa hadi Februari 8.
Korea Kaskazini imepuuzilia mbali ukosoaji wa mpango wake ikisema kuwa hakuna mtu aliye na uwezo wa kuishutumu.
''Ni
utamaduni na swala muhimu sana kwamba kila taifa duniani linasherehekea
uzinduzi wa jeshi lake' , kilisema chama tawala cha wafanyikazi Rodong
Sinmun.
Marekani imesema kuwa ingependelea gwaride hilo kutofanyika kwa kuwa kwa sasa watu wanalenga michezo ya Olimpiki.
Siku
ya Alhamisi, Korea Kaskazini ilisema kuwa haina mpango wa kukutana na
maafisa wa Marekani , kulingana na chombo cha habari nchini Korea
Kaskazini KCNA.
Serikali ya Korea Kusini imesema kuwa mwezi
uliopita kwamba wanajeshi 13,000 na vifaa 200 vilipatikana karibu na
uwanja wa ndege wa Pyongyang katika kile kinachoonekana kuwa gwaride la
majaribio.
Wataalam wanasema Korea Kaskazini inatarajiwa kuonyesha silaha zake za masafa marefu.
''Kile tunachotarajiwa kuona katika gwaride hilo la
kijeshi ni magari ya kubeba silaha, idadi yake na iwapo yanabeba silaha
mpya'' , alisema David Schmerler, mchanganuzi wa Korea Kaskazini katika
kituo cha James Martin cha masomo ya kuzuia kusambaa kwa silaha
No comments:
Post a Comment