Huduma za serikali ya Marekani
zimekwama baada ya bunge la Congress kushindwa kupitisha mkakati muhimu
wa bajeti yake kwa wakati unaofaa.
Wabunge walitumai kwamba watapitisha matumizi mapya kabla ya muda wa kufadhili bajeti hiyo kukamilika.
Lakini seneta wa Republican Rand Paul alimaliza matumaini ya kupigwa kwa kura ya haraka wakati alipoitisha mjadala bungeni kuhusu marekebisho ya matumizi.
Mnamo mwezi Januari , kisa kama hicho cha kushindwa kupitisha matumizi ya serikali katika wakati unaofaa kilisababisha serikali kuwa na mkwamo wa siku tatu.
Hatahivyo wafanyikazi wa serikali wameombwa kutumia maajenti wa nyumbani ili kupata ,mwelekeo kuhusu ni lini watarudi kazini.
Mabunge yote ya seneti na lile la uwakilishi ni sharti yaidhinishe matumizi hayo ya miaka miwili.
Mkwamo huo ulitarajiwa ikiwa imesalia saa moja kabla ya muda kukamilika wakati bunge la seneti lilipopiga kura ya mapumziko.
Lakini licha ya kuchleweshwa ,bunge hilo linatarajiwa kupigia kura matumizi hayo.
Bunge la uwakilishi halitapiga kura yoyote hadi pale bunge la seneti litakapoidhinisha matumizi hayo.
Haijulikani ni vipi bunge la Congress litaendelea na vile huduma za umma zitakavyoathirika.
Hatua hiyo itasababisha kupanda kwa matumizi hadi $300bn (£215bn) - Kitu ambacho seneta Paul anasisitiza hawezi kuunga mkono.
Huku ufadhili wa bajeti ya idara ya ulinzi ukionekana kuwafurahisha maafisa wa maswala ya usalama, wahafidhana wanapinga athari za deni la taifa hilo.
Seneta Paul aliyekasirika aliwakemea wenzake wa chama cha Republican akidai ufisadi unaoendelea.
''Niligombea wadhfa huu kwa sababu nilikuwa mkosoaji mkubwa wa deni la Trilioni za madola katika utawala wa rais Obama''.
No comments:
Post a Comment