Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepewa saa 48 kujiuzulu, wadhfa wake huo.
Kwa
mujibu shirika la Utangazaji la Afrika Kusini -SABC- na vyanzo vingine
vya habari, hatua hii inakuja baada ya mlolongo wa mazungumzo
yaliyofanywa na chama tawala cha nchini humo ANC.
Duru zinasema
ANC kilifanya mazungumzo marefu baadaye kuwatuma watu wawili nyumbani
kwa Rais Zuma jijini Pretoria kwenda kumfikishia ujumbe wa chama ana kwa
ana ya kwamba Zuma ajiuzulu mwenyewe au chama kimng'oe madarakani.
Lakini haijulikani bado kwamba Rais Zuma alipokeaje ujumbe huo.
Hatua hii ya ANC inaonekana ndio njia rahisi zaidi ya chama
hicho kumng'oa rais Zuma madarakani badala ya kusubiri utaratibu wa
bunge ambao ungeweza kuwa mrefu na wenye madhara zaidi kwa chama cha
ANC.
Rais Jacob Zuma ambaye anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya rushwa, alishindwa uongozi wa chama tawala Desemba mwaka jana.
Kiongozi
mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa anaongoza shinikizo za kumuondoa Zuma
katika nafasi yake hiyo ya Urais, na hatimaye kushika pia nafasi hiyo.
Ramaphosa
ameahidi pia kupambana na rushwa iliyokithiri na kukijenga upya chama
cha ANC, wakati nchi hiyo ikielekea katika uchaguzi mwakani.
No comments:
Post a Comment