Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amesema hali ya afya ya Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyepo nchini India inaendelea vizuri.
Kagaigai
amesema leo Februari 14,2018 kuwa Spika Ndugai yupo India kwa ajili ya
kuangalia afya yake (check-up) na anatarajiwa kurejea nchini wakati
wowote.
Katibu
huyo wa Bunge amesema, “Tulikwisha kusema kwamba Spika yuko India kwa
ajili ya ‘check-up’ na hali yake inaendelea vizuri.”
Alipoulizwa
kuwa Spika atakuwa ughaibuni hadi lini, Kagaigai amesema: “Hilo ni kati
ya daktari wake na yeye lakini ninachoweza kusema wakati wowote anaweza
kurudi nchini.”
No comments:
Post a Comment