Monday, February 5, 2018

MCHUNGAJI ELIZABETH AWAALIKA WATU KUHUDHURIA IBADA YA CHUO CHA MANABII SIKU YA KESHO JUMANNE.


Kadinali wa pili wa Huduma ya Ngurumo ya upako mchungaji Elizabeth Humphrey amewakumbusha watu wote kuhudhuria ibada ya chuo cha manabii siku ya kesho jumanne katika hema la kukutania kisongo arusha.

 Akizungumza na N.Y.U FM REDIO 99.3  siku ya leo mchana mchungaji Elizabeth amesema kuwa
"kesho hapo jumanne  itakuwa ni siku ya baraka sana ,uje ujifunze neno la mungu  sawa sawa na ambavyo mtu wa mungu ameachilia nguvu kubwa ya mungu ndani yetu,unapaswa kuja kukaa na kusikiliza neno la mungu  ili tuzidi kuimarika "amesema mchungaji Elizabeth.
 "lakini zaidi pia tunahuduma za ofisini jumatatu ,jumatano, ijumaa na jumamosi muda saa 09:30 asubuhi mpaka saa 04:30 jioni  kwa jumamosi ni saa 09:30 mpaka 12:30 mchana"
Ibada za chuo cha manabii ndani ya huduma ya ngurumo ya upako huwa ni ibada za katikati ya wiki ambazo ni kila siku ya jumanne na alhamisi kunzia saa sita kamili mchana na pia watu hupata nafasi ya kuhudumiwa kwa karibu zaidi na watumishi wa mungu wanaotumika chini ya mkono wa kinabii.

No comments:

Post a Comment