Tuesday, February 6, 2018

WATU WAKUMBUSHWA KUHUDHURIA IBADA YA CHUO CHA MANABII HII LEO JUMANNE

Kadinali wa pili wa Huduma ya Ngurumo Ya Upako mchungaji Elizabeth Humphrey amewakumbusha watu wote kuhudhuria ibada ya chuo cha manabii itakayofanyika hii leo kuanzia majira ya saa sita kamili mchana  katika hema la kukutania kisongo arusha.
 Akizungumza na N.Y.U FM REDIO 99.3  siku ya leo mchungaji Elizabeth amesema kuwa
"Hii leo jumanne  itakuwa ni siku ya baraka sana ,uje ujifunze neno la mungu  sawa sawa na ambavyo mtu wa mungu ameachilia nguvu kubwa ya mungu ndani yetu,unapaswa kuja kukaa na kusikiliza neno la mungu  ili tuzidi kuimarika "amesema mchungaji Elizabeth.
 "lakini zaidi pia tunahuduma za ofisini jumatatu ,jumatano, ijumaa na jumamosi muda saa 09:30 asubuhi mpaka saa 04:30 jioni  kwa jumamosi ni saa 09:30 mpaka 12:30 mchana"

Ibada za chuo cha manabii ndani ya huduma ya Ngurumo Ya Upako ibada za katikati ya wiki ni kila siku ya jumanne na alhamisi kunzia saa sita kamili mchana na pia watu wanapata nafasi ya kuhudumiwa kwa karibu zaidi na watumishi wa mungu wanaotumika chini ya mkono wa kinabii.

No comments:

Post a Comment