Kwa
mujibu wa kiongozi Mwandamizi wa chama cha MDC, Tsvangirai mwenye umri
wa 65, na aliyewahi kushika nafasi ya Uwaziri mkuu nchini Zimbabwe
ameripotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na Saratani ya utumbo.
Makamu
Rais wa chama chama cha MDC Elias Mudzuri ameliambia Shirika la Habari
la Uingereza Reuters kwamba marehemu alifariki jioni ya Februar 14.
Katika
kipindi cha uhai wake, maisha yake ya kazi yaligubikwa na harakati
nyingi za kisiasa dhidi ya mpinzani wake Rais wa zamani wa Zimbabwe
Robert Mugabe.
Aliwahi kupigwa na kufungwa mara kadhaa.
Morgan
Tsvangirai alianzisha chama cha Movement for Democratic Change -MDC-
mwaka 2000, na kuanza kutoa changamoto kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo
aliyekaa madarakani muda mrefu.
Kufuatia
kifo hicho Bwana Tsvangirai . MDC inaelekea kugawanyika juu ya nani
atakayeongoza uchaguzi hapo baadaye mwaka huu dhini ya chama tawala cha
Zanu PF, ambacho kwa sasa kinaongozwa na Emmerson Mnangagwa.
No comments:
Post a Comment