MAHAKAMA
ya Wilaya ya Dodoma imeagiza mkazi wa mtaa wa Ng’ong’ona Manispaa ya
Dodoma Tito Machibya, maarufu kama ‘Nabii Tito’ (45) kupimwa akili upya
katika Taasisi ya Afya ya Akili ya Mirembe Isanga mkoani Dodoma ili
kujiridhisha kama ana matatizo ya akili.
Licha
ya kuagizwa mtuhumiwa huyo kufanyiwa vipimo upya, mahakama pia imetaka
kuwasilishwa kwa vielelezo kama kweli ana tatizo hilo kama alivyoieleza
mahakama.
Nabii Tito anashtakiwa kwa kosa la kujaribu kujiua kwa kutumia wembe.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Karayemaha, alisema jana kuwa
kutokana na mshtakiwa kuieleza mahakama kuwa ana matatizo ya akili na
alifanya tukio hilo kutokana na kusikia vitu ambavyo vilikuwa
vinamwamuru akate, mahakama itabidi ipate vielelezo ambavyo
vitathibitisha anachokisema.
Karayemaha
alisema kutokana na kifungu namba 219 (2) cha Sheria ya Mwenendo wa
Mashauri ya Jinai, kama mshtakiwa atabainika kweli ana matatizo ya afya
ya akili, mahakama itaamua kuwa alivyofanya tukio hilo hakuwa na akili
timamu, hivyo hana hatia.
“Mshitakiwa
anadai kuwa ana matatizo ya akili na amekuwa akitibiwa katika hospitali
mbalimbli ikiwemo ya Maweni. Mahakama hii inaagiza vielelezo vyake
vyote viletwe hapa lakini pia apelekwe kwenda kufanyiwa uchunguzi wa
afya ya akili Mirembe Isanga,” alisema Karayemaha.
Pia
alisema kama mshtakiwa atabainika kuwa hana tatizo lolote la afya ya
akili kwa mujibu wa vielelezo vyake pamoja na vipimo atakavyofanyiwa,
atakuwa na kesi ya kujibu.
“Kutokana
na hili aliloiambia mahakama kuwa ana matatizo ya akili hata suala la
dhamana tunaliweka pembeni kwanza kwa sababu hawezi kujieleza lakini
kama itabainika kuwa hana matatizo ya akili kutokana na vielelezo
vitakavyoletwa pamoja na vipimo vitakavyofanyika, suala la dhamana
litafanyiwa kazi,"alisema.
Hata hivyo alisema mshtakiwa huyo anarudi rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa Februari 19, mwaka huu.
Wakati kesi itakapotajwa vielelezo vyote pamoja na vipimo vinatakiwa kuwa tayari vimeshawasilishwa mbele ya mahakama hiyo.
Nabii Tito anashtakiwa kwa tuhuma za kutaka kujiua kwa kujikata
No comments:
Post a Comment