Rais
John Magufuli amemuapisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed.
Luteni
Jenerali Mohamed ameteuliwa jana Februari 14, 2018 kuwa Mnadhimu Mkuu
wa JWTZ na kupandishwa cheo kutoka Meja Jenerali na kuwa Luteni
Jenerali.
Luteni Jenerali Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali, James Mwakibolwa ambaye amestaafu.
Mbali
na uteuzi huo, Rais Magufuli pia amewapandisha vyeo kutoka Brigedia
Jenerali na kuwa Meja Jenerali J.G. Kingu, M.S. Busungu, R.R. Mrangira,
B.K. Masanja, G.T. Msongole, A.F. Kapinga, K.P. Njelekela, A.S. Bahati,
M.E. Mkingule na S.S. Makona.
Taarifa ilitotolewa Ikulu jana imesema mabrigedia jenerali wote waliopandishwa vyeo watapangiwa vituo vya kazi baadaye.
Kabla
ya kuapishwa kwa Luteni Jenerali Mohamed, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
(CDF), Jenerali Venance Mabeyo aliwavalisha vyeo mameja jenerali
waliopandishwa vyeo na Rais Magufuli.
No comments:
Post a Comment