Katika
siku za karibuni kumejitokeza vitendo vya baadhi ya watu kutumia majina
ama picha za watu na kuwahusisha na matukio ya kihalifu au matukio
yanayohusiana na uhalifu kwa lengo la kujipatia umaarufu, kuwachafua
watu hao au kuwakosanisha na jamii inayowazunguka.
Mnamo
tarehe 11.09.2017 kupitia mitandao ya kijamii kulisambaa picha ya
askari wa Jeshi la Polisi akihusishwa na muendelezo wa tukio la
kujeruhiwa kwa risasi kwa Mhe. Tundu Lissu (MB) ambapo taarifa hiyo
ilimtambulisha askari huyo kuwa ni kachero wa Kitengo cha Interpol na
kwamba yupo jijini Nairobi nchini Kenya akifuatilia taarifa za Mhe.
Lissu.
Jeshi
la Polisi linapenda kukanusha taarifa hizo kuwa si za kweli na ni za
uongo zenye lengo la kumchafua askari huyo na Jeshi la Polisi kwa
ujumla.
Askari huyo hayupo Nairobi kama ilivyoenezwa na picha iliyotumika ilipigwa hapa nchini tarehe 07.01.2017 kwenye sherehe ya mahafali ya mtoto wa kaka yake.
Askari huyo hayupo Nairobi kama ilivyoenezwa na picha iliyotumika ilipigwa hapa nchini tarehe 07.01.2017 kwenye sherehe ya mahafali ya mtoto wa kaka yake.
Kuhusiana
na safari ya Nairobi, askari huyo alikuwa nchini Kenya kwa kozi ya
kimafunzo kuanzia tarehe 04.09.2017 na kurejea tarehe 08.09.2017, huku
Mhe. Lissu akipatwa na mkasa wa kujeruhiwa kwa risasi Tarehe 07.09.2017
na kusafirishwa kwenda Nairobi usiku wa kuamkia tarehe 08.09.2017.
Jeshi
la Polisi linakemea vikali kitendo hiki chenye lengo la kumharibia
maisha yake askari wetu, na linawataka wale wote waliohusika kusambaza
au kutajwa katika taarifa hizo kuripoti kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai (DCI) kwa ajili ya mahojiano.
Vilevile tunatoa onyo kwa wote wanaofikiri kuwa wanaweza kukaa na kupika habari ili waweze kuivuta jamii iwe upande wao na kuchafua upande wa serikali.
Vilevile tunatoa onyo kwa wote wanaofikiri kuwa wanaweza kukaa na kupika habari ili waweze kuivuta jamii iwe upande wao na kuchafua upande wa serikali.
Suala
hili la Mhe. Lissu lipo chini ya uchunguzi ili kuwabaini wote
waliohusika na tukio hili na hatimaye kuwafikisha mahakamani.
Ni vema wananchi na wanasiasa wakaliacha Jeshi la Polisi liweze kufanya kazi yake bila kuliingilia ili kuweza kupata ukweli wa jambo hili.
Ni vema wananchi na wanasiasa wakaliacha Jeshi la Polisi liweze kufanya kazi yake bila kuliingilia ili kuweza kupata ukweli wa jambo hili.
Jamii
itambue kuwa Jeshi la Polisi linafanyakazi kwa mujibu wa Sheria, kanuni
na taratibu za Nchi na kamwe halifanyi kazi kwa kuvizia.
Endapo mtu yeyote anahitaji taarifa, tunayo mifumo yetu rasmi inayotuwezesha kupata taarifa tuzitakazo kupitia uhusiano tulionao ndani na nje ya nchi.
Endapo mtu yeyote anahitaji taarifa, tunayo mifumo yetu rasmi inayotuwezesha kupata taarifa tuzitakazo kupitia uhusiano tulionao ndani na nje ya nchi.
Jeshi
la Polisi kupitia Kitengo cha upelelezi wa makosi ya mitandao (Cyber
Crime Investigation Unit) linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wote
waliohusika na kusambaa kwa taarifa hizi za uongo ili hatua za kisheria
zichukuliwe dhidi yao.
Jeshi
la Polisi linatoa rai kwa wananchi kuacha kutumia mitandao ya kijamii
vibaya na badala yake mitandao hii itumike kwa ajili ya kuelimisha na
kuihabarisha jamii juu ya masuala mbalimbali ya kimaendeleo.
Imetolewa na:
Barnabas David
Mwakalukwa – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
No comments:
Post a Comment