Waziri wa Maji na umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge amesema
Serikali inatekeleza ujenzi wa mradi wa bomba la maji safi kutoka ziwa viktoria
kuelekea katika mji wa Ngudu na vijiji vinavyopitiwa na mradi huo ili kuwapunguzia wananchi adha ya maji
wanayoipata.
Waziri Gerson Lwenge amesema hayo bungeni mjini Dodoma wakati
akijibu swali la Machimba Mashauri Ndaki mbunge wa Maswa Magharibi aliyetaka
kujua
ni lini serikali itakamilisha ujenzi wa mradi wa bomba la maji kutoka
Ziwa Viktoria.
Amesema kuwa serikali kupitia mpango wa sekta ya maji
imetekeleza mradi wa maji katika maeneo ya malampaka, Sayusayu, Masayi, Njia
panda na Senga mwarugesha ambayo maeneo hayo wananchi hupata maji huku akiongeza kuwa miradi ya
maji ya lalago, Mandhang’ombe na Jija ikiwa inaendelea kujengwa ambapo ujenzi
wake umefikia asilimia 65.
Aidha amesema kuwa Serikali imekamilisha usanifu na
makabrasha ya Zabuni kwa miradi ya maji ya Mwabulimbu, mwamanenge na Badi ambao
utahudumia vjiji vitatu vya Muhiba, Jibu na Badi huku akisema kuwa miradi hiyo itafanyika
katika awamu ya pili ya program ya maendeleo sekta ya maji.
No comments:
Post a Comment