Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo, Dk Harrison Mwakyembe ametoa
agizo kwa Watanzania kupuuza maneno ya upotoshaji yanayosemwa na watu
wachache hususani wanasiasa kuhusu ubovu wa ndege za Serikali aina ya
Bombardier.
Amesisitiza kuupuza habari hizo kwani anaamini kuwa wazushaji hao hawana utaalamu wowote wa kutambua jambo hilo.
Mwakyembe
alizungumza hayo pindi akifanya mahojiano na maalumu na waandishi wa
habari akiwa katika chumba cha abiria kwenye uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Songwe akijiandaa kusafiri kwenda Dar es salaam.
Dk
Mwakyembe amesema wapo watu wamekuwa wakipiga kelele za uzushi kwamba
serikali imenunua ndege mbovu, jambo ambalo siyo la kweli kwani mchakato
wa upatikanaji wa ndege hizo ulianza muda mrefu ukiwashirikisha
wataalamu mbalimbali kwa kuzingatia mazingira ya nchi pamoja na viwanja
vilivyopo.
“Kuna
watu wanasema ndege hizi ni mbovu sasa watuletee za kwao ambazo siyo
mbovu. Kwanza hawana hata utaalamu wa kujua ndege nzima au mbovu pia
wanachoangalia ni kutumia pangaboyi tofauti na zingine lakini ubora ni
uleule,”.
No comments:
Post a Comment