Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa yupo Nairobi nchini Kenya kumjulia hali
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyelazwa katika Hospitali ya
Aga Khan, baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.
Lissu
ambaye pia ni mwanasheria wa Chadema alijeruhiwa kwa risasi tano
Alhamisi Septemba 7 akiwa ndani ya gari nyumbani kwake Area D mjini
Dodoma akitokea bungeni.
Katika
akaunti yake ya Twitter, Lowassa ame-tweet akisema, “Earlier today i
paid a visit at Nairobi Hospital to see our MP, President of TLS and
dear friend @tundulissutz He is recovering well. It is Sad times for
Tanzania. Let us all keep praying.”
Kwa
tafsiri isiyo rasmi amesema “Mapema leo nilitembelea Hospitali ya
Nairobi kumwona mbunge, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika
(TLS) na rafiki kipenzi Tundu Lissu. Anaendelea vizuri. Ni kipindi cha
masikitiko kwa Tanzania. Kwa pamoja tuendelee kuomba.”
Katika
tweet hiyo, Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, ameweka
picha akiwa pamoja na Alicia ambaye ni mke wa Lissu; Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe na dereva wa Lissu Simon Mohamed Bakari.
No comments:
Post a Comment