Mbunge
wa Sengerema, William Ngeleja amehojiwa kwa saa moja katika Ofisi ya
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), jijini Dar es Salaam leo Jumatatu
Septemba 11.
Ngeleja
ambaye pia amewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini wa awamu ya nne,
aliwasili katika ofisi hiyo saa nne asubuhi akiwa peke yake ambapo
alikutana na DCI saa tano na kuondoka saa sita na nusu mchana bila
kusema alichohojiwa.
Hatua
ya Ngeleja kufika ofisini hapo ni kuitikia wito wa Mkuu wa Jeshi La
Polisi (IGP), Simon Sirro ambaye aliwataka watuhumiwa waliotajwa katika
ripoti ya Tanzanite na Almasi kuripoti kwenye ofisi hiyo kwa ajili ya
mahojiano wakati uchunguzi ukiendelea
No comments:
Post a Comment