Jeshi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo (jana) limetimiza miaka 53 tangu
kuanzishwa kwake ambapo akiongeza na waandishi wa habari Jenerali mabeyo
aliwaambia waandishi kuwa yuko na Jenerali Sarakikya (rtd) Mkuu wetu wa
Majeshi ya Ulinzi wa Kwanza Mzalendo, Jenerali Mwamunyange (rtd) Mkuu
wa Majeshi wa Saba, ambaye nimepokea kijiti hiki toka kwake mwezi
Februari, 2017.
Wapo
pia, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Mwakibolwa, Mkuu wa Jeshi
la Kujenga Taifa Meja Jenerali Isamuhyo, Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa
Matawi (Machifu) wa Makao Makuu ya Jeshi na Sajini Meja wa Jeshi letu.
Nimeona
nijumuike nao wote hawa ili kwa pamoja kupitia kwenu Waandishi wa
Habari mtuwasilishie salamu zetu za Maadhimisho ya Miaka 53 ya JWTZ, kwa
Watanzania wote. Maadhimisho haya yalianza tarehe 25 Agosti, 2017 kwa
Wanajeshi wote kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo Michezo,
kufanya Usafi kwenye maeneo ya kijamii na Tiba. Leo hii tunahitimisha
Madhimisho hayo.
Siku
hii ya leo JWTZ linasherehekea kutimiza miaka 53 tangu kuundwa kwake
Septemba Mosi, 1964. Hii ni siku muhimu sana kwetu na kwa wananchi wa
Tanzania kwa ujumla, kwa sababu, JWTZ ni Jeshi letu sote na limeundwa
kutokana na Wananchi wa Tanzania. Awali ya yote kwa heshima na taadhima
ninapenda kutumia fursa hii kumshukuru sana Rais wetu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt John Pombe
Joseph Magufuli kwa kuniamini na kuniteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi. Pili kwa niaba ya JWTZ na kwa niaba yangu mwenyewe napenda
kumshukuru Waziri wa Ulinzi na JKT, pamoja na Wizara anayoiongoza kwa
mwongozo anaotupatia na ushirikiano mkubwa anaoutoa kwa Jeshi.
Aidha,
Wakati tunatimiza Miaka 53 napenda pia kuwashukuru Baraza la Mawaziri
pamoja na Viongozi Wakuu wa Serikali kwa Maelekezo mbalimbali
wanayoyatoa kwa Jeshi letu. Ushauri wao umekuwa mhimili mkubwa kwa
utendaji wa Jeshi letu. Ninawashukuru pia Wakuu wa Majeshi Wastaafu,
wengine ninao hapa leo mnawaona kwa namna walivyolilea Jeshi letu katika
nyakati mbalimbali hadi hii leo tunatimiza miaka 53 likiwa Jeshi kubwa
kabisa, lenye nidhamu kubwa, weledi na uhodari mkubwa.
Wakati
tunaandika Historia ndefu ya Miaka 53, Jeshi letu limefikia mafanikio
mbalimbali, miongoni mwa mafanikio ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ)
ni kudumisha amani na utulivu uliopo nchini mwetu tangu Taifa letu
lipate Uhuru wake. Aidha, JWTZ limeshiriki Vita vya ukombozi Kusini mwa
Afrika, Vita vya Kagera na Visiwa vya Comoros. Jeshi letu pia limekuwa
ni nguzo muhimu katika kudumisha amani sehemu mbalimbali duniani kwa
kushiriki katika shughuli za Ulinzi wa Amani, katika nchi za Liberia,
DRC, Sudan (Darfur), Lebanon, Sudan Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati
n.k. Ndani ya Nchi Jeshi letu limeshiriki kutoa usaidizi katika masuala
mbalimbali ikiwemo majanga, uokoaji na huduma za kijamii. JWTZ bado
limeendeleza mshikamano na kuonesha uzalendo wa hali ya juu na hivyo
kubakia kuwa Jeshi la Wananchi.
Naomba
niwatakie Maafisa na Askari wa JWTZ na Watanzania kwa ujumla “Happy
Birthday”. Ninawapongeza sana kwa kufikia siku ya leo. Kwa vile leo ni
siku ya Eid El Hajj nawatakia Eid Njema pia wao na familia zao.
Mwisho,
ninawaomba watanzania wote waliunge mkono Jeshi lao na JWTZ daima liko
imara na tayari kuilinda Nchi yetu. Tutailinda na kuitetea Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa uaminifu Serikali
yetu. Namuomba Mungu atusaidie.
JENERALI VENANCE SALVATORY MABEYO, ndc
MKUU WA MAJESHI YA ULINZI
No comments:
Post a Comment