Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambayo inajukumu
la kusajili, kuratibu na kufuatilia uendeshaji wa shughuli za Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali nchini imeamua kuongeza muda wa siku 16 kwa
Mashirika ambayo bado hayajahakiki taarifa zake kwa Msajili wa
Mashirikka yasiyo ya Kiserikali kukamilisha uhakiki huo.
Akizingumza
na waandishi wa Habari Mjini Dodoma jana Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo
ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga alisema kuwa kumekuwa na mwitikio mkubwa wa
Mashirika yasiyo ya kiserikali kuja kuandikisha taarifa za asasi zao
katika vituo mbalimbali vya usajili vya kanda.
Bibi
Sihaba aliongeza kuwa Serikali ina nia njema ya na siyo mbaya kama watu
wanavyohisi katika utekelezaji wa zoezi hili la uhakiki linaloendelea
nchi nzima katika vituo vya Kanda tano (5), na lengo ni la zoezi ni
kutambua takwimu halisi ya Mashirika yanayofanya kazi ili kuweka
utaratibu mzuri wa kutambua mchango wa kila asasi katika kuhudumia jamii
katika nyanja mbalimbali.
“Niwaombee
wadau wetu watumie muda huu tuliouongeza vizuri kwa kujitokeza kwa
wingi kufanya uhakiki wa Mashirika yao na wale wenye changamoto
tutawaelekeza namna bora ya kuzitatua,” alisema Bibi Sihaba.
Aidha
Msajili wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Bw. Marcel Katemba
aliwahikikishia wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini kuwa
hakuna tatizo katika zoezi la uhakiki wao na ni muhimu sana kujihakiki
ili kujiwekea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao kwa uhuru na uwazi.
“
Niwahakikishie wadau wetu kuwa zoezi hili ni muhimu sana kwenu na kwetu
pia katika namna ya kuboresha utendaji kazi wetu,” alisema Bw. Katemba.
Naye
Katibu wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini Bw. Ismail
Suleiman ameishukuru Serikali kuwa kuandaa na kuratibu zoezi la uhakiki
wa mashirika hayo na kuwaomba wamiliki wa mashirka yasiyo ya kiserikali
nchini kujitokeza kuhakiki mashirika yao.
“Niwaombe
wamiliki wa Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini tuendelee kujitokeza
kwa wingi tuje tuhakiki mashirika yetu ili tuondokane na usumbufu mara
baada ya kumalizika kwa kuda wa uhakiki ulioongezwa,” alisema Bw.
Ismail.
Zoezi
la uhakiki wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini lilizinduliwa na
katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Agosti 21,2017 na uhakiki huo ulitekelezwa kwa muda wa wili mbili mpaka
Septemba 04,2017.
Hata
hivyo kutokana na sababu za kijiografia na mwitikio mkubwa wa mashirika
kutaka kuhakikiwa ikaamuliwa kuongeza kwa muda wa siku 16 mpaka
Septemba 20 mwaka huu, ambao ndio utakuwa mwisho wa uhakiki.
No comments:
Post a Comment