Uongozi
wa Kampuni ya Williamson Diamonds Limited (WDL) umesitisha kwa muda
baadhi ya shughuli za uzalishaji katika mgodi huo.
Taarifa
ya uongozi wa mgodi huo kwa wafanyakazi jana, zilisema huduma za
uzalishaji zimesimamishwa isipokuwa huduma maalumu za ulinzi, tiba,
umeme, maji, zimamoto na usafiri unaohitajika katika huduma hizo.
Taarifa
hiyo ilisema huduma za utawala zitaendelea kufanya kazi wakati huduma
nyingine zitakazoendelea kuendeshwa na mgodi itatolewa taarifa
uzalishaji utakaporejea.
Taarifa
hiyo ilisema Kampuni ya WDL inasubiri agizo la kuacha kusafirisha
nje almasi yake kutoka mgodini, kifurushi namba W1-FY18.
Hata
hivyo, taarifa za ndani zinasema Serikali imezuia kusafirisha kifurushi
hicho kwa misingi ambayo haijawasilishwa rasmi kwao licha ya kuona
taarifa hizo kupitia vyombo vya habari.
“Hatuwezi kutoa maoni yoyote kutokana na matokeo ya uchunguzi huo.
“Vifurushi
vyote vinavyosafirishwa kwa biashara nje hukadiriwa thamani yake hapa
mgodini na watumishi wa ‘TANSORT’ ambacho ni kitengo cha kukadiria
thamani ya almasi na vito wanaowawakilisha Wizara ya Nishati na Madini.
“Kifurushi
kinavyosafirishwa kinapigwa mihuri miwili ya vyombo viwili vya
Serikali, sisi uongozi hatuna ujuzi wanaoutumia ‘TANSORT’ wa kukadiria
kwa muda malipo ya mrabaha kwa Serikali.
“Yanakamilishwa
baada ya kupatiwa matokeo halisi ya zabuni ya wazi ya almasi za WDL na
uaminifu wake unathibitishwa na TANSORT kutoka wizarani,’’ilieleza
sehemu ya taarifa hiyo.
Kamishna
wa Nishati na Madini, Benjamin Mchwampaka jana alisema taarifa ya
mgodi huo haijafika kwake bali ameiona kwenye mitandao ya jamii.
Alisema
mpaka sasa hawezi kujua athari za kusimamisha uzalishaji wa mgodi huo
hadi atakapopata taarifa rasmi kutoka kwa uongozi.
“Nimeziona mitandaoni, sijapata taarifa kutoka kwao wenyewe itabidi kuitafakari ikifika kesho (leo).
“Lazima
niweze kujua hilo na niweze kufahamu pia athari na wamefunga maeneo
gani na athari hata kwa wafanyakazi itakuwa kwa kiasi gani ,’’alisema
Mchwampaka.
Hivi
karibuni wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA), walikamata mzigo wenye madini ya almasi yenye uzito wa kilo
29, dakika tano kabla ya ndege kupaa, huku yakiwa yameandikwa yana kilo
14.3.
Inaelezwa
walioshiriki kufanya udanganyifu huo ni watumishi wa serikali
waliopewa dhamana ya ukaguzi na uthaminishaji katika mchakato wa
kuanzia mgodini hadi kuidhinisha usafirishaji wa madini hayo nje ya
nchi.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango, juzi alitembelea uwanja wa JNIA
kwa ajili ya kutoa maagizo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka (DPP),
Mganga Biswalo.
Alisema Tanzania imepigwa vya kutosha hivyo wote waliohusika katika udanganyifu huo washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.
Waziri
alisema wafanyakazi wote waliohusika kuanzia hatua ya uchimbaji wa
madini hayo mpaka kule yanakosafirishwa, wamulikwe na vyombo vya dola
kubaini uhalali wa mali zao wanazomiliki.
Ilielezwa
kuwa wamiliki wa mgodi wa madini hayo walisema yana thamani ya Dola za
Marekani milioni 14.8, lakini baada ya uchunguzi ilibainika thamani
yake ni Dola za Marekani milioni 29.7.
No comments:
Post a Comment