Mbunge
wa Iringa Mjini (Chadema) Msigwa ameachiwa huru jana usiku kwa dhamana
baada ya kukamatwa akiwa kwenye mkutano wa hadhara.
Msigwa
aliachiwa baada ya kudhaminiwa na wadhamini wawili Alex Kimbe pamoja na
Mwenyekiti wa Bavicha Iringa Leonce Marto , saa nne usiku .
Msigwa
alishushwa jukwaani kwa nguvu akiwa anahutubia mkutano wa hadhara
katika kata ya Mlandege Manispaa ya Iringa na anatuhumiwa kwa kosa la
uchochezi dhidi ya vyombo vya usalama .
Marto
amesema mikutano yake imefungiwa na hapaswi kuendelea na ziara yake
katika kata nyingine mpaka hapo OCD atakapo amua vinginevyo.
Leo
Mbunge anatakiwa kuripoti kwa RCO na huenda kesi ya uchochezi ambayo
tayari imeshafunguliwa jalada lake ikapelekwa mahakamani .
Amesema
Mbunge huyo atazungumza na vyombo vya habari leo mchana kuweka wazi
madhila yaliyompata wakati akitekeleza wajibu wake kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment