Mwenyekiti
wa kamati ya Spika iliyochunguza uchimbaji wa almasi, Azzan Mussa Zungu
amesema vita ya kupigania rasilimali za nchini imewaunganisha wabunge
wa vyama vyote.
Kamati
hiyo iliyoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai ilipewa jukumu la
kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini
ya almasi nchini.
Zungu
ambaye ni mbunge wa Ilala, amesema leo Septemba 7 kuwa wabunge wote
wanatamani rasilimali za Tanzania zitumike na Watanzania na si kuwapa
furaha wawekezaji kutoka nje.
“Kamati
ilipoenda Shinyanga ilibaini upungufu mkubwa katika usimamizi wa madini
yanayochimbwa na hata wachimbaji wanapofanya ndivyo sivyo, bodi ya
almasi haichukui hatua yoyote,” amesema Zungu.
Amesema bodi ya almasi imewaangusha Watanzania kwa kushindwa kusimamia vizuri madini hayo ya vito kama ambavyo imepewa dhamana.
“Mgodi
wa almasi uliopo Shinyanga umekuwa kama shamba la bibi, viongozi wa
Serikali walikuwa wanaenda kule kuchota fedha na kugawana,” amesema.
Amesema hayo wakati wa kukabidhi ripoti kwa Rais John Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment