Rais
Magufuli amewataka viongozi mbalimbali wa serikali ambao wametajwa
kwenye ripoti za bunge ya madini ya Almasi na Tanzanite wamepishe nafasi
zao ili vyombo vya usalama viweze kufanya kazi yake vizuri
kuwachunguza.
Rais
Magufuli amesema hayo leo wakati akikabidhiwa ripoti hizo Ikulu jijini
Dar es Salaam na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kusema amesikia baadhi
ya viongozi mbalimbali wengine ambao amewateuwa yeye kuwa wameusishwa
kwenye wizi huo hivyo amewataka wapishe.
"Wako
watu wametajwa tajwa, na wengine mimi ndio nilihusika kuwateua sasa
ukishatajwa tajwa, naagiza vyombo vya ulinzi na usalama vifuatilie hili
tena kwa haraka.
"
Wale ambao wametajwa tajwa kwenye ripoti hii ambao ni wateule wangu,
ili vyombo vya usalama viweze kufanya kazi yake vizuri, ni matumaini
yangu watakaa pembeni" alisema Rais Magufuli
Katika
ripoti hiyo ambayo iliwasilishwa jana mjini Dodoma na leo kukabidhiwa
kwa Rais Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa iliweza kuwataja baadhi
ya viongozi wa serikali ikiwepo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za
mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. George Simbachawene, Waziri wa
zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja
pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo.
No comments:
Post a Comment