Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji ameamua kwenda kuripoti Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar
Taarifa
iliyotolewa leo Jumatatu na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya
Chadema, Tumaini Makene imesema Dk Mashinji ameambatana na wasaidizi
wake kutoka makao makuu ya chama hicho.
“Katibu
mkuu amewasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam,
kuitikia wito wa Polisi uliotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,
Gilles Muroto, kuwa anatakiwa kufika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai (DCI)” amesema.
Awali, leo Jumatatu Dk Mashinji alisema hawezi kwenda kuripoti kwa kuwa hakuambiwa siku maalumu ya kwenda.
Kamanda
Muroto amemtaka Dk Mashinji afike ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai
mkoani Dodoma au ofisi kama hiyo iliyopo Kituo Kikuu cha Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam ili kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kuhusu
tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu
Lissu.
“Nina
taarifa za kuitwa Polisi, lakini haziko ‘specific’. Ni wakati wowote
naweza kwenda? na hawajasema nikaripoti wapi. Kwa hiyo, wakinihitaji
watakuja kuniambia,” alisema Dk Mashinji leo asubuhi.
Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mchana alipokuwa akielekea nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.
Kwa sasa Lissu anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi, Kenya.
No comments:
Post a Comment