Spika
wa Bunge, Job Ndugai amesema Shirika la Madini la Taifa (Stamico) ni
muhimu, hivyo Wizara ya Nishati na Madini inapaswa kulitazama upya kuona
namna ya kuliboresha ili liwe jipya kwa kuwa limewaangusha Watanzania.
Ndugai
amesema hayo leo Septemba 7 Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati wa
kukabidhi kwa Rais John Magufuli ripoti za kamati alizoziunda kutathmini
mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya
tanzanite na almasi.
Spika
amesema wawekezaji wengi wanaokuja nchini ni wazuri lakini wakikuta
mifumo ya kuwasimamia ipo ovyo nao huanza mambo ya ovyo.
“Kamati
zote zinazungumzia mikataba ambayo ni ya kawaida sana. Kikubwa
Watanzania tuwe wazalendo na kushikamana. Wakati wa Mwalimu Julius
Nyerere alijaribu kupingania rasilimali zetu ikafika hatua dawa ya meno
ikakosekana madukani lakini Watanzania waliendelea kumuunga mkono,” amesema Ndugai.
No comments:
Post a Comment