Aliyekuwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa , George Simbachawene ambaye amejiuzulu nafasi yake hiyo kufuatia agizo la Rais kuwataka watu waliotajwa kwenye ripoti ya Tanzanite na Almasi kupisha, amefunguka na kujitetea
Simbachawene amefunguka na kusema kuwa amehushishwa kwenye sakata hilo
kwa kuwa alihudumu katika wizara hiyo na kusema lakini yeye hakuhusika kwa lengo la kuhujumu uchumi wa taifa wala hakuwa na lengo baya kwa nchi.
"Kampuni ambayo ilikuwa na ubia na serikali iliamua kumuuzia mtu mwingine ili aje kufanya kazi na serikali kwa hiyo zilikuwa ni 'private arangement' ambazo lazima wazilete serikalini sasa hata kama angebaki yule wa mwanzo au huyu alichukua bila shaka matokeo ya kutokuwa na faida katika uendeshaji wa rasilimali hii yangekuwa ni yale yale, kwa hiyo uhusika wangu na kutajwa kwangu bila shaka ni kwa sababu nilihudumu kwenye wizara ile lakini nina imani ya dhati ya moyo wangu kwamba uhusika wangu haukulenga kuhujumu taifa, haukuwa wa maslahi binafsi bali ni katika majukumu ya kiutendaji" alisema Simbachawene Tangu Rais Magufuli ametoa kauli hiyo ya kuwataka wateule wake wote ambao wamehushishwa kwenye ripoti hizo mbili za madini zilizoundwa na Spika Job Ndugai kupisha ni mawaziri wawili wamethibitisha kufanya maamuzi hayo akiwepo Simbachawene pamoja na aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani.
No comments:
Post a Comment